26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Barca, Griezmann kimeeleweka rasmi

CATALUNYA, Hispania

Rasmi mabingwa wa Ligi Kuu Hispania, La Liga, Barcelona wamefanikiwa kupata saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa, Antoine Griezmann kwa kiasi cha pauni milioni 107.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alihusishwa kujiunga na miamba hiyo ya Catalunya tangu alipotangaza kuondoka Atletico Madrid mwezi Mei, hadi leo Barcelona walipotangaza rasmi baada ya kuachia kipande cha video kikimuonesha Griezmann akiwa amevalia jezi ya timu hiyo ikisindikizwa na maneno yanayosema “Ulikuwa unasubiria hili”.

Griezmann ataitumikia Barcelona miaka mitano hadi Juni mwaka 2024 ambapo atakuwa anaingiza pauni milioni 15 ambazo ni sawa na bilioni 38 za Tanzania kwa mwaka kiasi ambacho kimeongezeka kuliko alichokuwa anapata Atletico Madrid.

Nyota huyo wa Ufaransa, anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na mabingwa hao baada ya kiungo wa Ajax, Frenkie de Jong ambaye ada yake ilikuwa pauni milioni 63  sawa na bilioni 180 za Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles