24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

BARAZA VYUO VIKUU LAJIPANGA KUKABILI SOKO LA AJIRA

Na Christina Gauluhanga-Dar es Salaam


 

profesa-kirimi-kiriamitiBARAZA la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki limesema linafanya jitihada kuhakikisha wanashirikiana na sekta binafsi kutoa wanafunzi bora wanaouzika katika soko la ajira .

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Kirimi Kiriamiti, alikuwa akizungumza   Dar es Salaam jana kuhusu kongamano la siku mbili litakalowakutanisha washiriki  zaidi ya 170 kutoka baraza hilo na sekta binafsi.

Alisema malengo ya kongamano hilo ni kujadili mbinu  na mifumo mbalimbali ya elimu inayotolewa ili kuzalisha wanafunzi bora wanaouzika katika soko la ajira.

Alisema kongamano hilo litasaidia waajiri na wanavyuo mbalimbali kupitia utafiti ulioibuliwa na wanafunzi hao na kuona namna ya kuiendeleza.

“Tunahitaji kuzungumza lugha moja na waajiri ili kutoa wanafunzi wanaouzika katika soko la Afrika Mashariki kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi,”alisema Kiriamiti.

Alisema upo utafiti mwingi wenye maslahi kwa taifa lakini umeshindwa kuendeleza hivyo ni imani hii fursa itasaidia kutoa mwanya kwa watafiti mbalimbali.

“Upo utafiti umefanywa na una matokeo mazuri ila kwa sababu ya ukosefu wa fursa na fedha mwingi umeshindwa kuendelezwa,”alisema Kiriamiti.

Alisema pia baraza hilo limepanga kuanzisha vituo maalum vya mafunzo mbalimbali ambavyo vitapanua weledi kwa wanafunzi wa kufanya utafiti utakaosaidia kuinua uchumi wa nchi.

Makamu Mkuu wa Chuo cha St. Johns Dodoma, Emmanuel Mmbene, ambaye pia ni mjumbe wa kamati tendaji ya baraza hilo, alisema kongamano hilo litasaidia kulinda soko la ndani.

Alizitaja nchi zinazoshiriki katika konganano hilo kuwa ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles