25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

BAO LA BOCCO LAFUNIKA MABAO SITA YA OKWI

Na THERESIA GASPER -DAR ES SALAAM

BENCHI la ufundi la klabu ya Simba, limeridhishwa na umahiri wa ufungaji uliotumiwa na mshambuliaji, John Bocco, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Mwadui FC.

Bao la mshambuliaji huyo ambaye amesajiliwa na klabu ya Simba akitokea Azam msimu huu, limeonekana kufuta thamani ya mabao sita yaliyofungwa na mchezaji, Emmanuel Okwi.

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC, kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini hapa.

Akizungumza na MTANZANIA juu ya bao hilo, kocha mkuu, Joseph Omog, alisema mchezaji huyo ameifungia  Simba bao zuri tangu kuanza kwa msimu huu.

“Nimependa bao alilofunga Bocco kwani alionekana kupambana na kufanikiwa kulifunga kiufundi zaidi,” alisema Omog.

Upande wake kocha msaidizi, Jackson Mayanja, alisema Bocco amefunga bao ambalo si la kawaida, hivyo anastaili kupongezwa ukizingatia ni mchezaji mgeni katika timu.

“Bocco amefungua ukurasa wa mabao, amefanikiwa kufunga bao bora tena kiufundi, tunaamini ataendelea kutoa dozi kwenye mechi zote,” alisema Mayanja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles