23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

DYANA NYANGE AJIANIKA KWA YEMI ALADE

Na JESSCA NANGAWE

MKALI wa ngoma ya ‘Chovya’, Dyana Nyange,  amefunguka na kudai sasa ni wakati wake wa kutoboa kimataifa ili kukuza muziki wake zaidi, huku akipanga kumshirikisha staa wa Nigeria, Yemi Alade.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake hicho, amesema wimbo huo umezidi kumtambulisha zaidi na umeifunika ile ngoma ya Komela.

Akizungumza na MTANZANIA, msanii huyo alisema tayari amefanya kazi na mtayarishaji wa muziki nchini Afrika Kusini, Captain Blue na kazi hiyo itaanza kuonekana hivi karibuni.

“Nadhani sasa ni wakati wangu wa kufanya kazi kimataifa zaidi na tayari nimeanza kazi hiyo baada ya kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki wa Afrika Kusini, pia nipo kwenye mipango ya kuwashirikisha mastaa wakubwa kama  Yemi Alade na wengine, lengo ni kupanua wigo zaidi wa kazi zangu,” alisema Dyana Nyange.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles