25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

BANGLADESH YAKANA KUWAREJESHA WAROHINGYA MYANMAR

DHAKA, BANGLADESH


SERIKALI ya Bangladesh jana ilikana madai ya Myanmar kuwa taifa hilo lenye wakazi wengi waumini wa dini ya Buddha limewarejesha nyumbani wakimbizi watano.

Wakimbizi hao wa familia moja walidaiwa kuwa miongoni mwa Warohigya 700,000 waliokimbilia hapa kukwepa machafuko yaliyoongozwa na Jeshi la Myanmar dhidi ya jamii hiyo ya wachache.

Awali Jumamosi, taarifa ya Serikali ya Myanmar ilisema watu watano wa familia moja wamerejeshwa katika jimbo la magharibi la Rakhine kutoka katika eneo la mpaka.

Taarifa hiyo imesema familia hiyo ilikuwa ikiishi kwa muda na ndugu zao katika mji wa Maungdaw, mji mkuu wa jimbo hilo karibu na mpaka na Bangladesh.

Lakini Waziri wa Mambo ya Ndani wa Bangladesh Asaduzzaman Khan alisema madai ya Myanmar kwamba familia hiyo imerejeshwa si ya kweli, na kudokeza kwamba familia hiyo haijawahi kufika katika ardhi ya Bangladesh.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles