24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

BANGI YARUHUSIWA CANADA

Matumizi ya bangi kwa kujiburudisha yatahalalishwa nchini Canada ifikapo tarehe mosi Julai mwaka 2018.

Serikali ya Canada itawasilisha muswada wa kuhalalisha bangi ifikapo Aprili kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CBC.

Taarifa ziliiambia CBC kuwa wanachama wa chama tawala cha Liberal hivi majuzi walijulishwa kuhusu muswada huo.

CBC imesema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo lililoteuliwa na serikali.

Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa Canada itaruhusu kuuzwa kwa bangi wa kujiburudisha kwa watu walio na zaidi ya umri wa zaidi ya miaka 18.

Jopo hilo pia lilipendekeza kuwa watu wazima wataruhusiwa kupanda hadi mimea minne ya bangi na wamiliki hadi gramu 30 ya bangi iliyokaushwa.

Kwa mujibu wa CBS, serikali itasimamia kusambazwa wa bangi na kuwapa leseni wazalishaji.

Kwa upande mwingine, mwaka jana Desemba wapiga kura katika majimbo ya California na Massachusetts waliidhinisha matumizi ya bangi (marijuana) kwa kura.

Kura ya kuidhinisha matumizi ya mmea huo iliyopigwa sambamba na ile ya uchaguzi wa rais, iliidhinisha kisheria uzalishaji na matumizi ya bangi kwa watu wenye umri wa miaka 21.

Wapigaji kura katika majimbo mengine waliopigia kura kuidhinisha kwa matumizi ya bangi kwa ajili ya kujifurahisha ni Arizona, Maine, na Nevada, ambako matokeo bado hayajajulikana.

California ilisema ushuru juu ya mauzo na kilimo cha bangi utasaidia kuboresha mipango ya vijana, mazingira na utekelezwaji wa sheria.

Vilevile, mwaka jana huo huo mwezi Septemba, kundi moja la wabunge nchini Uingereza lilitoa wito wa kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi kwa sababu za kimatibabu nchini humo.

Kundi hilo linalojumuisha wabunge kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa, na ambalo limekuwa likitetea mageuzi kuhusu matumizi ya dawa, lilisema kuna ushahidi bayana kwamba matumizi ya bangi huwa na manufaa katika kutibu baadhi ya matatizo ya kiafya, yakiwemo maumivu makali na kutatizwa na wasiwasi.

Kwa mujibu wa wataalamu, mmea wa bangi huwa na karibu kemikali 60. Lakini Taasisi ya Taifa ya Afya Uingereza imetahadharisha kwamba bangi huwa na madhara makubwa kwa mwili, ikiwemo kutatiza uwezo wa mtu kuendesha gari na kudhuru mapafu na afya ya kiakili, kuathiri uwezo wa mtu kuzaa na kuathiri pia watoto ambao hawajazaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles