Balozi Andrey Karlov alipigwa risasi na askari polisi mjini Ankara,Uturuki aliyekuwa akipaza sauti akitaja kulipiza kisasi cha yanayojiri Aleppo.
Askari huyo aliyejulikana kwa jina la Mevlut Mert Altintas aliuliwa pia na polisi katika mapambano yaliyodumu kwa muda wa dakika 15 na katika tukio hilo, watu wengine watatu waliumizwa.
Tukio la kuuwawa kwa Karlov ambaye alikuwa balozi wa Urusi nchini Uturuki, wengi wamelihusisha na maswala ya kigaidi kwani haikujulikana dhahiri kuwa nia yake ilikuwa ni nini lakini alichokifanya kimefanana na namna magaidi hufanya matukio yao.
Hata hivyo, Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Moscow amesema Uturuki wamehakikishiwa kwamba kutakuwa na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo na wote watakaokuwa wamehusika wataadhibiwa.
Meya wa Ankara amesema mauwaji hayo yamelenga huharibu mahusiano ya nchi hiyo na Urusi. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry amesema Marekani iko tayari kusaidia katika uchunguzi wa tukio hilo.