Na MWANDISHI WETU-RUANGWA
BARAZA la Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), linafanyika leo wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Kuadhimishwa kwa sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume, kulitanguliwa na Maulid yaliyosomwa usiku wa kuamkia leo wilayani hapa, katika Viwanja vya Shuele ya Sekondari Likangala.
Taarifa ilitotolewa na Bakwata, ilieleza kuwa kabla ya kusomwa kwa maulidi hayo, jana jioni ilifanyika zafa (maandamano) makubwa na kuongozwa na Madrasat za Zubairiyya na Daarul Maarifa kutoka jijini Dar es Salaam.
baada ya kusomwa kwa maulidi leo litafanyika Baraza la Maulidi, wilayani hapa ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd huku mwenyeji wa hafla hiyo akiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa.
Katika sherehe hiyo ya maulidi viongozi mbalimbali watahudhuria wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally.
Pia watakuwepo Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Bakwata, Sheikh Hamis Mataka, Kaimu Katibu Salum Abeid, Mjumbe Baraza la Ulamaa Sheikh Himid Jongo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, Â Shamim Khan pamoja na Mkurugenzi wa Elimu Ali Ali.
Wengine ni masheikh kutoka mikoa mbalimbali pamoja na Katibu na Mwenyekiti wa Vijana Bakwata, Alhaj Muharami Pembe na Katibu wake Alhaj Sheikh Athuman Zubeir na maofisa wengine waandamizi