27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi Italia azindua Swahili Fashion Week

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

Balozi wa Italia nchini, Marco Lombardi, amezindua nembo ya msimu wa 14 wa tamasha la mitindo ‘ Swahili Fashion Week’, linalotarajia  kufanyika  kuanzia Desemba 3-5, 2021 jijini Dar Es Salaam.

Tamasha hilo limekuwa likifanyika kila mwaka na kukutanisha wabunifu na wanamitindo kutoka nchi mbalimbali za ndani na nje ya Afrika

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo juzi usiku katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Balozi huyo amesema nchi ya Itali, ipo pamoja  na uongozi wa Swahili Fashion Week kuhakikisha wanafanikisha tamasha hilo kwa mara nyingine.

Wanamitindo

“Imekuwa ni kawaida ya nchi yetu kudhamini tamasha hili kwa sababu tunatambua sekta ya ubunifu wa mavazi inatoa ajira kwa kasi kwa watu wa rika tofauti na kukuza uchumi wetu,” anasema Lombardi.

Kwa upande wake mratibu wa jukwaa hilo, Benedict Msofe amesema wabunifu zaidi ya 50 wamejisajili kuonyesha kazi zao mwaka huu katika tamasha hilo.

“Mwaka huu kumekuwa na  mwamko mkubwa kwa sababu ya wabunifu wengi wamejitokeza kushiriki katika jukwaa hili kuonyesha kazi zao pamoja na kuuza katika hoteli ya Serena ambapo ndipo panapofanyika tamasha hili mwaka huu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles