27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Bale apanga kufanya makubwa El Clasico

BaleMADRID, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale, amedai kwamba katika mchezo wa El Clasico uliopita dhidi ya Barcelona hakuwa katika ubora wake, lakini kwenye mchezo huu ujao atawashangaza mashabiki.

Katika mchezo wa awali, Madrid walikuwa kwenye Uwanja wa nyumbani, Santiago Bernabeu na kukubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya wapinzani wao, Barcelona. Jumamosi ya wiki hii Madrid wanawafuata Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp, huku wakiwa na lengo la kulipa kisasi.

“Najua katika mchezo wa awali dhidi ya Barcelona sikuwa kwenye ubora wangu, lakini kwa sasa nipo vizuri na ninaamini nitawashangaza mashabiki kwa kile ambacho nitakifanya.

“Tunaujua ubora wa wapinzani wetu, lakini hakuna wasiwasi kwa kuwa kila kitu kinawezekana kwa upande wetu, tunaweza kufanya makubwa kwa kuwa kwenye kikosi kuna wachezaji ambao wana uwezo mkubwa.

“Barcelona kwa sasa inaongoza Ligi, lakini hata sisi bado tuna nafasi ya kuwa mabingwa kutokana na michezo iliyobaki na kama wapinzani wetu watapoteza michezo yao ijayo,” alisema Bale.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, aliweka rekodi ya usajili wake mwaka 2013, ambapo alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 85.3 akitokea Tottenham.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles