26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

BAKWATA WAOMBA SERIKALI KUHARAKISHA UPELELEZI KESI ZA UGAIDI

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeviomba vyombo vya dola kuharakisha upelelezi wa kesi za ugaidi ili haki itendeke kwa wakati.

Mwishoni mwa mwaka jana baraza hilo lilitahadharisha kuwa suala la ugaidi linaweza kutumiwa kama njia ya kulipiza visasi katika jamii na kusababisha raia wema wasio na hatia kuhusishwa na vitendo hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, alisema haki inatakiwa ionekane inatendeka na kitendo cha kuichelewesha ni sawa na kumnyima mtu haki yake.

“Sio masheikh tu bali waumini wote wanaohusishwa na kesi za ugaidi, tunaomba upelelezi uharakishwe ili kesi zilizokaa muda mrefu ziweze kufikia mwisho, na watakaoonekana wana hatia wahukumiwe na wasio na hatia waachiwe huru na kuendelea na shughuli zao,” alisema.

Alisema Katiba imetamka wazi kwamba mtu yeyote atabaki kuwa mtuhumiwa hadi mahakama itakapothibitisha kosa lake. Hivi karibuni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislam ya Imam Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, aliwataka waislamu wote nchini kuungana na kupigania haki za masheikh na waislamu waliopo magerezani.

Mwezi uliopita pia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alimtaka Rais Dk. John Magufuli kutafakari upya juu ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho ambao wanasota gerezani kwa zaidi ya miaka minne sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles