24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Babu mbaroni akituhumiwa kumpa mimba mjukuu wake wa miaka 13

NA TIGANYA VINCENT-TABORA

JESHI la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mzee wa miaka 67 kwa tuhuma za unyanyasi wa kijinsia na kusababisha ujauzito kwa mtoto wa miaka 13 ambaye ni mjukuu wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, ACP Barnabas Mwakalukwa alisema Novemba 13, mwaka huu, mama mzazi wa mtoto huyo  aligundua kuwa binti yake anayesoma darasa la sita Shule ya Msingi Kizigo iliyopo Manispaa ya Tabora  ni mjamzito.

Kamanda Mwakalukwa alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Said Tumaini ambaye ni mganga wa kienyeji na mkazi wa Kizigo, Manispaa ya Tabora.

Katika tukio jingine, jeshi hilo limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali ambavyo vinadhaniwa kuwa ni vya wizi, baada ya watu waliokuwa wamevipakia katika pikipiki tatu kuvitelekeza na kukimbia.

Kamanda Mwakalukwa alivitaja vitu vilivyokamatwa ni runinga tatu, komputya, friji, redio tano na spika zake, pikipiki mbili zenye usajili wa MC 545 AGZ, MC 224 AXL na nyingine ambayo haina namba.

Alisema msako dhidi ya watu hao waliotoroka na kuacha pikipiki na vitu hivyo unaendelea na kuwataka wenye taarifa zao kuzitoa polisi.

Kamanda Mwakalukwa alisema watafanya uchunguzi kubaini wamiliki wa pikipiki hizo na kutoa wito kwa wahusika kujisalimisha kabla hawajakamatwa.

Wakati huo huo, jeshi hilo limefanikiwa kumkamata Joyce Seth na Emmanuel Shayo wote wakazi wa Kiloleni mkoani Tabora wakiwa na mtambo mmoja na lita 120 za pombe haramu ya gongo.

Kamanda Mwakalukwa alisema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali dhidi ya wahalifu na watu wote watakaokutwa wakizurura kuanzia saa sita usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles