Baba wa Babu Tale azikwa Mkuyuni Morogoro

0
1318

TaleNA THERESIA GASPER
BABA mzazi wa Meneja wa Abdul Nassib ‘Diamond’, Babu Tale, amezikwa jana kijijini kwao Mkuyuni, mjini Morogoro.
Baada ya mazishi hayo, baadhi ya wasindikizaji walirejea jijini Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao na mipango mingine ya kumaliza msiba.
Msanii wa kundi hilo, Madee, alisema baada ya mazishi wote watarejea jijini Dar es Salaam, ambapo itasomwa dua ya kuhitimisha msiba huo nyumbani kwa Babu Tale, Magomeni Kagera.
“Tupo njiani kuelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi ya baba yetu mpendwa, tukimaliza tutarudi Dar es Salaam kwa ajili ya mipango mingine,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here