23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Baba mzazi wa Eminem afariki dunia kwa matatizo ya moyo

Fort Wayne, Marekani

Baba mzazi wa Rapa Marshall Bruce Mathers III maarufu Eminem, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 67 kwa maradhi ya moyo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mtandao wa TMZ zinasema mzee huyo ambaye jina lake ni Marshall Bruce Mathers Jr’67 alifariki akiwa nyumbani kwake katika mji wa Fort Wayne, Indiana nchini Marekani.

Taarifa zinasema kuwa Eminem hakuwahi kuwa na ukaribu na baba yake mzazi hii ni baada ya wazazi wake kutengana akiwa bado na miezi sita ambapo taarifa za awali ziliwahi kusambaa kuwa Marshall alikuwa akimnyanyasa mke wake Deborah R. Nelson-Mathers ambaye ni mama yake rapa huo na kupelekea hadi wawili hao kuachana.

Eminem akiwa na mama yake mzazi

Eminem aliwahi kusema hakuwahi kumuona baba yake zaidi ya kuona picha zake na aliwahi kumuandikia barua ili kujenga ukaribu lakini hazikuwahi kujibiwa ambapo Marshall aliibua malalamiko kwa mama mzazi wa Eminem na kusema kuwa yeye ndiye sababu ya kutokuwepo na maelewano baina yake na mwanae.

Aidha kutokuwepo kwa maelewana kati yake na baba yake ndio chanzo cha nyimbo za ke nyingi ikiwa ‘Out My Closet’ iliyokuwa inapatikama katika albam ya Deezer iliyotoka mwaka 2002.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles