Baba Haji: Pacho amenifundisha vingi

0
3029

Patch+blogNA GEORGE KAYALA, DAR ES SALAAM
MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’, amesema kupata nafasi ya kufanya kazi na Pacho Mwamba kumemsaidia kujifunza vitu vingi.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Baba Haji alisema kwa muda mrefu alikuwa amejiwekea malengo ya kufanya kazi na msanii huyo maarufu wa muziki wa dansi nchini.
Alisema tayari maandalizi ya filamu hiyo ambayo imepewa jina la ‘Mary Mary’, yamefikia hatua nzuri, hivyo mashabiki wajiande kupokea ujio wake mpya.
“Filamu yangu mpya itaingia sokoni mwezi ujao, nimeweza kumshirikisha msanii mwingine, Miriam Ismail, ambaye ameonyesha kufanya vizuri,” alisema Baba Haji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here