Katika gazeti letu la Mtanzania toleo No. 7709 la Alhamisi Januari 22, mwaka huu, tuliandika kimakosa stori yenye kichwa cha habari ‘Wema Sepetu ampeleka Diamond Polisi’. Baada ya kufanya uchunguzi tumejiridhisha habari ile haikuwa na ukweli, kwani chanzo kilichotupatia kilitupotosha, hivyo kuleta usumbufu kwa msanii Wema pamoja na jamii. Kutokana na hali hiyo, tunapenda kumwomba radhi Wema na familia yake. Siku zote sisi MTANZANIA tumekuwa makini katika kusimamia misingi ya habari za weledi na haki kwa jamii.