26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yamnasa kinara wa mabao Chan

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KATIKA kuhakikisha inaondokana na ukame wa mabao,Azam imemalizana na mshambuliaji kutoka katika klabu ya Highlanders ya nchini Zimbabwe, Prince Dube.

Hatua hiyo inalengo la kuifanya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuwa moto zaidi.

Msimu uliopita,Azam ilipachika 52, huku mshambuliaji Obrey Chirwa, akiwa kinara wa mabao katika kikosi hicho baada ya kutupia mabao 12.

Kutokana na hilo, Azam iliamua kumfungia safari Dube Zimbabwe kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo.

Nyota huyo ameitumikia timu ya taifa ya Zimbabwe katika michezo tisa na kufungua mabao manne.

Benchi la ufundi la Azam chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba linaamini atakuwa na msaada mkubwa akishirikiana na Chirwa pamoja na Never Tigere.

Chanzo kutoka Azam Complex kililiambia  MTANZANIA jana kuwa, timu hiyo tayari imekubaliana kimaslahi na Dube na kusaini mkataba wa miaka mitatu.

“Viongozi wameshamalizana na Dube wakiingia nae mkataba wa maika miwili na muda wowote atawasili Tanzania kuanza majukumu yake.

“Azam walikuwa wanamuhitaji mchezaji huyu tangu kipindi cha usajili wa dirisha dogo lakini mkataba wake ulimzuia kufanya mazungumzo na hata mabosi wake hawakuwa tayari kumuachia.

Safari hii wamefanikiwa kumuondoa Highlanders baada ya kulipa dola elfu 50 kwa ajili ya uhamisho wake,”kilisema chanzo hicho.

Msemaji wa Azam FC, Zakaria Thabiti alipoulizwa kuhusiana na habari hiyo, hakuweza kukiri kama wamefanikiwa kumsajili mchezaji huyo, lakini anakubali kwamba wanasaka straika mkali kutoka nje ya Tanzania.

“Tunahitaji mshambuliji kutoka nje ya Tanzania atakayekuja kusaidiana na hawa waliopo ili kutupa mabao mengi, wapo wastraika wawili tumezungumza nao, mmoja wapo atawasili nchini wakati wowote kwa sababu tumekamilisha mipango yote kwa asilimia 99, kama ni Dube au nani itajulikana baadae,”alisema Zakaria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles