24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yaiporomosha Yanga kileleni

azamNA JENIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

TIMU ya Azam FC imeitibulia Yanga kwa kuitoa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya  kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 na kukwea juu yao katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Azam wamefikisha pointi 35 wakiishusha Yanga nafasi moja ambao wana pointi 33 katika msimamo wa ligi hiyo.

Lilikua bao la mshambuliaji John Bocco, ambalo lilitosha kuirejesha Azam kileleni, baada ya kufunga bao pekee la ushindi dakika ya 86.

Bocco alifunga bao hilo baada ya kupiga shuti la moja kwa moja, lililotokana na mpira wa adhabu baada ya Shabani Nditi kumchezea rafu Kipre Tchetche nje ya 18.

Hata hivyo, katika mchezo huo uliokua wa kukamiana hadi kufikia dakika 15 za kwanza, timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu lakini hakuna hata moja iliyoweza kuona lango la mwenzake.

Bocco alikosa bao dakika ya 29 baada ya kupiga shuti lililotokana na mpira wa kona uliopigwa na Farid Mussa na kutoka nje.

Hadi dakika ya 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika kwa mwamuzi Damian Mabena, kupuliza kipenga kuashiria mapumziko, hakukuwa na timu yoyote  iliyoona lango la mwingine.

Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu ambapo dakika ya 57, Mtibwa walikosa bao la wazi kupitia kwa mchezaji wake Shiza Kichuya, aliyeambaa na mpira tangu katikati ya uwanja na kujikuta akizidiwa nguvu na kipa wa Azam, Aishi Manula na mpira kutoka nje.

Azam baadaye waliongeza nguvu kwa kufanya mabadiliko dakika ya 55, alitoka Faridi Mussa na kuingia Ramadhani Singano.

Azam FC: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Abdalah Kheri, Lacine Diof, Pascal Wawa, Jean Mugiraneza, Frank Domayo, Salum Abubakar, John Bocco, Didier Kavumbagu na Faridi Salim.

Mtibwa Sugar: Said Mohamed, Ally Shomari, Issa Rashid, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Henry Joseph, Said Bahanuzi, Mzamiro Yassin, Boniface Maganga, Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles