23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Azam Tv yashusha neema Bongo Muvi

NA JEREMIA ERNEST

KAMPUNI ya Azam Media leo imetambulisha tamthilia nne za Kitanzania, moja ikiwa ya vichekesho na zitaanza kurushwa kuanzia Jumatatu wiki ijayo katika chaneli ya Sinema Zetu.

Tamthilia hizo zinaitwa Tunu, muandaaji ni Jenipha Kiyaka ‘Odama’, Mimi ya Elizabeth Michael ‘Lulu’,
Saluni ya mama Kimbo, muandaaji Abduli Usanga, Haikufuma ya Jacob Steven ‘JB’ na Mihemko vichekesho ya Haji Salum ‘Mboto’.

Akizungumza na wandishi wa habari leo,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando, amesema wamechukua kazi za wasanii wa hapa nchini ili kuinua sanaa ambayo kwa sasa imekua ikifanya vizuri.

“Hii ni awamu ya pili kuchukua kazi nyingi kwa wakati mmoja, hii ni fursa kubwa kwa wasanii wetu kuonyesha kazi zao pamoja na kuelimisha jamii ukizingatia kwa sasa sanaa ni ajira inayotambulika,” anasema Tido.

Aliongeza kuwa huu ni muda wa kufanya kazi, hivyo wasanii waepukane na maneno yasiyojenga tasnia kama kuna tatizo ni vizuri kufuata utaratibu wa kulitatua.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Azam Tv, Sabrina Mohamedali’s, amesema kwa sasa wadau wa tamthilia wanaweza kuangalia kwa kutumia simu za mkononi kupitia App ya Azam Tv Max.

“Endapo utakuwa umechelewa kurudi nyumbani au upo mbali na Tv unaweza kufatilia vipindi vyetu kwa kutumia simu ya mkononi pia visimbusi vyetu vinavyo tumia antena,tayari vimeshaingia sokoni katika jiji la Dar es Salaam.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles