26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 26, 2024

Contact us: [email protected]

Aweso aagiza wananchi kuunganishiwa maji kwa mkopo

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kuwaunganishia maji kwa mkopo wananchi ambao hawana uwezo.

Aweso ametoa maagizo hayo Novemba 17,2023 wakati wa utiaji saini mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam (mradi wa maji Bangulo).

Amesema mwananchi anayeomba kuunganishiwa maji isizidi wiki mbili na kama hana fedha akopeshwe aweze kupata huduma hiyo.

“Maji hayana mbadala, anayekosa maji madhara yake ni makubwa, hali tunatofautiana kama kuna mwananchi anashindwa kulipa mkateni katika bili yake kidogo kidogo lakini muunganishieni maji,” amesema Aweso.

Kuhusu mradi huo amesema utagharimu Sh bilioni 42 na kuwanufaisha wakazi zaidi ya 450,000 wa Jiji la Dar es Salaam na kumtaka mkandarasi kuutekeleza kwa kasi kwa kuwa fedha zipo.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Kiula Kingu, akizungumza wakati wa utiaji saini mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam.

Amesema mkandarasi huyo Kampuni ya Sinohydro ya China amefanya kazi nzuri katika miradi kadhaa ukiwemo wa Arusha uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 520 na kusisitiza asimamiwe kikamilifu ili mradi ukamilike kwa wakati.

Waziri huyo pia ameipongeza Dawasa kwa kazi nzuri ya utekelezaji miradi ya maji na kuielekeza bodi ikae na kupendekeza anayefaa kuwa mtendaji mkuu.

“Dawasa ni nguzo ya zege, tunajivunia mnafanya vizuri, endeleeni kufanya kazi kwa umoja na mshikamano na kutekeleza dhamira ya mheshimiwa Rais Samia ya kumtua mama ndoo kichwani,” amesema Aweso.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Kiula Kingu, amesema mradi huo utatekelezwa kwa miaka miwili hadi Oktoba 2025 na chanzo cha maji katika mradi huo ni mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu.

“Mradi huu unalenga kutatua changamoto za maji katika majimbo ya Ukonga, Segerea, Temeke, Kibamba na sehemu chache za jimbo la Kisarawe. Utakapokamilika utaongeza upatikanaji huduma za maji hadi kufikia asilimia 95 ifikapo mwaka 2025,” amesema Kingu.

Kwa upande wao wabunge wa majimbo ya Temeke (Doroth Kirave), Kibamba (Issa Mtemvu) na Segerea (Bonnah Kamoli) wamemshukuru Rais Samia kwa utekelezaji wa mradi huo ambao utaondoa kero ya upatikanaji maji kwa wapigakura wao.

“Tutamlipa mheshimiwa rais mwaka 2025 ushindi ambao haujawahi kutokea, hili la maji linatosha kutuvusha 2025,” amesema Mtemvu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles