MKALI wa muziki nchini Kenya, Judith Nyambura ‘Avril’, amewashangaza watu kupitia akaunti yake ya Instagram
baada ya ‘kuposti’ picha ambayo inamuonesha kuwa amefunga ndoa.
Tangu Januari mwaka huu, msanii huyo alitangaza kufunga ndoa na mpenzi wake kutoka nchini Afrika Kusini ifikapo Juni, mwaka huu, lakini mipango ikagonga mwamba, akatangaza ifikapo Novemba mwaka huu kila kitu kitakuwa sawa, hata hivyo mipango ikawa sio.
Lakini juzi kupitia mtandao huo wa Instagram, aliweka picha akiwa na mpenzi huyo huku wakionekana kuwa
wanafunga ndoa, lakini ya kitamaduni.
Hata hivyo, wawili hao kwa sasa wapo nchini Dubai kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Krismasi na ndipo inaonekana kuwa zoezi hilo limekamilikia huko.