27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Sauti Soul wachukua tuzo ya utanashati Afrika Mashariki

sauti-solKAMPALA, UGANDA

KUNDI la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol, wanazidi kujitengenezea jina baada ya juzi kufanikiwa kuchukua tuzo ya kundi bora la wasanii watanashati Afrika Mashariki.

Tuzo hizo zilitolewa Kampala, nchini Uganda, kwenye ukumbi wa Abryanz Style, ambapo tuzo hizo zilipambwa na wasanii mbalimbali kufanya shoo.

Kundi hilo kwa sasa limekuwa na jina kubwa mara baada ya kuanza kutajwa kwenye tuzo za MTV EMA mwaka 2014, MTV MAMAs na BET, hivyo tuzo hiyo ambayo wameipata juzi inawaonesha kwamba wao ni bora.

“Tunaweza kusema tunamaliza mwaka vizuri kwa kuchukua tuzo mbalimbali, lakini hii yote inatokana na kujituma kwetu na kushirikiana vizuri na wadau mbalimbali, kwa pamoja tunasema asante,” waliandika kupitia akaunti yao ya
Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles