23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Aveva ampa masharti mazito MO

DewjiNA MSHAMU NGOJWIKE

UONGOZI wa Simba upo tayari kumpa timu bilionea, Mohamed Dewji (MO), endapo wanachama watakubali kuuza hisa za klabu katika mkutano mkuu utakaofanyika Januari mwakani na kama atakubali kutoa thamani halisi ya klabu hiyo.

Hivi karibuni bilionea huyo alinukuliwa na vyombo vya habari akieleza nia yake ya kutaka kuimiliki klabu hiyo kwa kununua hisa za wanachama kwa asilimia 50 kwa kutoa ofa ya shilingi bilioni 20 za Kitanzania.

Akizungumza jijini jana, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema kuwa uongozi huo hauna shida na jambo hilo la kheri la kumkabidhi timu Dewji, ili aweze kuiendesha kisasa endapo ataweza kufanya mchanganuo mzuri wa thamani halisi ya klabu ya Simba.

“Sisi hatuna tatizo kwa vile tunahitaji kuiona Simba ikiendeshwa kisasa zaidi, lakini ni vizuri taratibu zikafuatwa hasa ikizingatiwa kwamba Simba ni mali ya wanachama,” alisema.

“Lakini pia anatakiwa kutoa gharama halisi za klabu maana Simba si majengo tu bali ina rasilimali zinazohitaji kujadiliwa kwa undani zaidi na jambo hili si la kukurupuka,” alisema Aveva.

Alisema jambo hilo ni zuri endapo likifanikwa kutokana na klabu hiyo kwa sasa imekuwa ikifanya matumizi makubwa tofauti na kipindi cha zamani ambapo mpira ulikuwa wa ridhaa.

“Simba sasa hivi tunatumia bajeti ya bilioni 1.5 hadi mbili, tofauti na zamani ambapo mpira ulikuwa wa ridhaa ila sasa mpira ni biashara na ongezeko la thamani limepanda.

“Lakini kwa bajeti hii imekuwa haikidhi mahitaji yote, maana kama unataka uweze kuingia katika ushindani basi inabidi utumie zaidi ya bilioni nne ama tano.

“Sisi Simba tunatumia mishahara ya wachezaji na matumizi mengine zaidi ya milioni 62 kwa mwezi, wakati wadhamini wetu wanatoa milioni 35 sasa hizi nyingine tunatoa wapi? Lazima tuingie katika dili hili,” alisema Aveva.

Alisema katika jambo hilo, Dewji atakuwa na upinzani mkali kutokana na kutokea mtu wa pili Mwanasimba pia ambaye ametenga zaidi ya bilioni 25 za kuinunua Simba.

Simba imekuwa ikipata matokeo mabaya katika mbio zake za kutafuta ubingwa katika misimu mitatu mfululizo, tangu ilivyoweza kubeba kwa mara ya mwisho msimu wa 2011/12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles