22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Kerr atupia zigo la lawama nyota wake

kerrNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa timu ya Simba, Dylan Kerr, amewatupia lawama nyota wake kuwa ndio chanzo cha mwenendo mbaya wa klabu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kauli ya Kerr imekuja siku chache baada ya tetesi za kutumuliwa kwake kuzidi kushika kasi, kutokana na matokeo yasiyoridhisha ambayo yamekuwa yakiiandama timu hiyo katika siku za karibuni.

Simba inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na jumla ya pointi 24, hadi sasa imefanikiwa kucheza mechi 12 tangu kuanza kwa msimu wa 2015/2016

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kerr alisema amekuwa akifanya kila jitihada za kuwapa mbinu za ushindi wachezaji wake, lakini anashindwa kuamini matokeo wanayopata.

“Ninajitahidi kufundisha kadiri ya uwezo wangu, hakuna mbinu ambayo sijaitumia kuwanoa wachezaji wangu, lakini kila wanapoingia uwanjani tunavuna kile tusichotarajia.

“Hakuna kocha anayefurahia matokeo mabaya kwa timu yake, hata mimi naumia sana ila mambo yanazidi kuwa tofauti hatusongi mbele tunazidi kurudi nyuma,” alisema.

Kerr alieleza yeye kama kocha uwezo wake wa kufundisha umefikia hapo, hivyo kuboronga kwao kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji wenyewe.

“Mnajiandaa vizuri na kila mchezaji mazoezini anaonyesha kiwango cha hali ya juu, lakini tunapofika uwanjani kila kitu kinaenda tofauti kabisa hayo si makosa yangu, mimi natambua wazi kuwa natimiza majukumu yangu kama mwalimu,” alisema Kerr.

Simba imeshindwa kutimiza malengo yake ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu mitatu mfululizo, imejikuta ikipoteza pointi sita katika mechi tatu, timu hiyo imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mwadui FC mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni mwendelezo wa matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Toto Africans na 2-2 dhidi ya Azam FC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles