Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital
Baada ya kutambulishwa rasmi leo, kiungo mpya wa Yanga Mganda, Khalid Aucho, amesema amejiunga na timu hiyo akiamini ni sehemu atakayocheza soka kwa furaha na kujiamini kwa sababu ni kama familia yake.
Akizungumza wakati akitambulishwa, Aucho, amesema kuna timu nyingi zilikuwa zikimhitaji ambazo zimepitia kwa wakala wake lakini Yanga walimuendea hewani mwenyewe.
Amesema ana mapenzi na Yanga, pia wakati wanamfuatilia alikuwa akizungumza vizuri na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Hersi Said ambaye ni kama mwanafamilia kwake.
“Nimekuja Yanga kwa mapenzi yangu na timu, waliongea na mimi mwenyewe kama mwanafamilia, lakini timu nyingine zilipitia kwa wakala,” amesema.