SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (UEFA) limemfungia mwamuzi aliyechezesha aliyeipa penalti Atletico Madrid katika mchezo dhidi ya AC Milan uliomalizika kwa Wahispania kushinda mabao 2-1.
Timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1 lakini UEFA wanasema mwamuzi Cuneyt Cakir alipaswa hakujidhirisha kwa VAR na badala yake aliamuru penalti ipigwe kuelekea kwa Milan kwa madai Pierre Kalulu aliunawa mpira kwenye boksi.
Hata hivyo, penalti hiyo iliyoipa Atletico ushindi wa mabao 2-1 imeonekana kuwa na makosa kwani marudio ya video yameonesha Thomas Lemar wa Atletico alishaunawa mpira kabla ya kumfikia Kalulu.
Penalti inayozungumziwa hapo ni ile aliyopiga Luis Suarez na mbali ya kosa hilo, yalikuwapo makosa kadhaa ya mwamuzi, ikiwamo kadi nyekundu aliyopewa kiungo wa Milan, Franck Kessie.