26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Askofu Chengula wa Kanisa Katoliki afariki dunia

PATRICIA KIMELEMETA-Dar es Salaam



ASKOFU wa Jimbo Katoliki Mbeya, Evaristo Chengula, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuugua kwa muda mfupi maradhi ya moyo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tec), Padre Dk. Charles Kitime, alithibitisha kufariki kwa Askofu Chengula na kusema taratibu za mazishi   zinaendelea.

“Ni kweli Askofu Chengula amefariki dunia  baada ya kuugua kwa muda mfupi.

“Juzi tulimpokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kumpeleka moja kwa moja Muhimbili kwa ajili matibabu, lakini Mungu amempenda zaidi, tumuombee,”alisema Dk. Kitime.

Alisema kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya mazishi wakimaliza watatoa taarifa lakini anatarajiwa kuzikwa kwenye Kanisa Kuu la Jimbo la Mbeya kama ilivyo utaratibu wa mazishi ya maaskofu.

Askofu Chengula  alizaliwa mwaka 1941 na alikuwa padre wa Shirika la Mtakatifi Consolata.

Aliwekwa daraja la uaskofu mwaka 1997 na mpaka anafariki dunia alikua askofu wa jimbo hilo.

Katika uhai wake, Askofu Chengula aliwahi kuwashauri vijana kujiunga na vyama vya siasa  kuleta haki na amani na siyo mihemko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles