22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU ASEMA AMANI IKO MIKONONI MWA VIJANA

Na BENJAMIN MASESE-UKEREWE

MWENYEKITI Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jiji la Mwanza, Askofu Charles Sekelwa, amesema maendeleo na ustawi wa Tanzania unategemea nguvu ya vijana na akina mama katika ujenzi wa amani.

Askofu Sekelwa alitoa kauli hiyo juzi, wakati akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro kwenye kongamano la maadili na uzalendo lililofanyika wilayani Ukerewe kwa ufadhili wa Taasisi ya Al Jaziira Islamic Centre.

Alisema kama Watanzania wataishi kwa kuzingatia uzalendo, mshikamano na kuhubiri amani hususan vijana, Tanzania itaepukika na matukio mabaya yanayoshuhudia katika mataifa mbalimbaliwa na kusababisha raia wake kuwa wakimbizi.

Hata hivyo Askofu Selekwa ambaye aligusia mgogoro ambao uliibuka mwaka 2013 jijini mwanza juu ya waumini gani wanapaswa kuchinja mifugo, alisema tukio halipaswi kujirudia kwani ni hatari sana katika usalama na ustawi wa taifa  ndani jamii  yoyote.

“Katika ujenzi wa miundombinu ya amani, maadili na uzalendo kwa nchi yetu lazima makundi ya vijana na akinamama ambao ndio mhimili mkubwa wa maendeleo na ustawi wa nchi wasiachwe bila kuwapa elimu hii. Watanzania tutakuwa tunafanya makosa makubwa  tukiyaacha makundi haya katika kujenga amani na mshikamano wa nchi yetu.

“Hili nalisema kwa sababu makundi haya ndiyo yenye nguvu katika jamii, sasa tusipowatanguliza katika kuhubiri amani na uzalendi itakuwa shda kidogo hapo mbeleni, hata ule mgogoro wa dini gani inapaswa kuchinja haupaswi kujirudia ndio maana Serikali ilituomba watu wa dini tukae tuondoe ile hali tete ambayo kwa namna moja ilikuwa inataka kusambaa nchi  nzima,”alisema.

Akifungua kongamano hilo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Oswald   Bankobeza, alisema mmomonyoko wa maadili umechangia kuharibu mambo mengi kwenye jamii na hivyo kongamano hilo liwe chachu ya kuayarejesha ili taifa liwe na watu waadilifu.

“Watanzania hawa wanahitaji amani na niwaombe  watu wa  dini endeleeni  kutuombea huku mkikifanya kazi ya kuisaidia serikali, sasa mmegeuka na kuanza kuihudumia jamii yote ili kuhakikisha amani mnayoihubiri iendelee kudumu,” alisema Bankobeza ambaye ni Mkuu wa Magereza Wilaya ya Ukerewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles