24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Askari watatu na raia wakiri makosa sita ya utakatishaji fedha kwa DPP

Mwandishi Wetu, Arusha

Askari watatu pamoja na raia watano, akiwepo Meneja wa Kampuni ya kuuza madini ya Crown Lapidary, Lucas Mdeme, waliokuwa wanashitakiwa kwa kumteka mfanyabiashara wa madini, Sammy Mollel na kumuomba rushwa ya Sh milioni 30, wamekiri mashataka sita.

Washitakiwa hao wameandika barua ya kukiri makosa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) wakikiri makosa ni ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu na kupanga njama za kujipatia fedha kinyume na, utaratibu ambapo awali walishachukua kiasi cha Sh milioni 10 kati ya Sh milioni 30 walizohitaji kutoka kwa Mollel.

Wakili wa watuhumiwa hao, Charles Kagirwa, ametoa taarifa hiyo jana Februari 10, wakati kesi ilipofikishwa mahakamani kwa kutajwa. Kesi hiyo imetajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Arusha, Rose Ngoka.

Hata hivyo, Hakimu Ngoka amesema hana taarifa za barua hiyo na ameiahirisha kesi hiyo mpaka Februari 24, kwa ajili ya kutajwa.

Kabla ya kupandishwa kizimbani Askari watatu walishtakiwa kijeshi na kufukuzwa kazi kwa kosa la kupokea rushwa ambao ni Askari mwenye namba G. 5134 DC Heavenlight Mushi aliyekuwa Askari kitengo Cha Intelijensia Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, H.125 PC Gasper Paul kitengo Cha Intelijensia Makao Makuu Dodoma na H.1021 PC Bryton Murumbe aliyekuwa Askari wa kawaida mkoani Dodoma.

Raia waliopandishwa mahakamani ni Mdeme Joseph Chacha(43) mkazi wa Iliboru, Leonila Joseph (46) mkazi wa Ilboru, Mfanyabishara maarufu Jijini Arusha ,Nelson Lyimo{58} mkazi wa Kijenge Juu na Omary Alphonce(43) mkazi wa Olasiva jijini Arusha.

Watuhumiwa wote walirudishw Mahabusu katika gereza la kisongo kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana hadi Februari 24.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles