29.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 30, 2024

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Askari mbaroni kwa kumuunguza mwanafunzi kwa pasi ya umeme

LNa ALLAN VICENT-TABORA

JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia askari wake, Koplo Almas mwenye namba E.9301, kwa tuhuma za kumuunguza mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Cheyo, Jumanne Hussein (17), kwa pasi ya umeme sehemu mbalimbali za mwili.

Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emanuel Nley, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 20, mwaka huu Mtaa wa Lumaliza, Kata ya Mbugani Manispaa ya Tabora.

Nley alisema mwanafunzi huyo alikutwa karibu na nyumba ya Koplo Almas akidaiwa kutaka kufanya mapenzi na binti wa askari huyo. 

Alisema baada ya kumkuta na binti yake alimkamata na kuanza kumuunguza kwa pasi ya umeme kisha kumpiga na kitu kizito kwenye paji la uso na mdomoni na kumjeruhi.

Alisema baada ya polisi kupata taarifa za mwanafunzi huo kuunguzwa, walimkamata Koplo Almas na hadi sasa anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi na atashtakiwa kijeshi kisha kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

“Tunamshikilia askari wetu E.9301 Koplo Almas kwa tuhuma za kumuunguza kwa pasi ya umeme na kumjeruhi vibaya mwanafunzi aliyemkuta na binti yake nje ya nyumba wakitaka kufanya mapenzi,” alisema.

Pia alisema tayari wamemchukulia hatua za awali za kinidhamu askari huyo kwa kumshtaki jeshini kutokana na shambulio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles