30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Asasi yahamasisha Watanzania kujitokeza kupiga kura kwa wingi

NA MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

ASASI ya The Right Way (TRW), imewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi Oktoba 28 mwaka huu ili wapige kura kwa uhuru kwakuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imeweka mazingira mazuri ya watu kushiriki zoezi la upigaji kura.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya watazamaji wa uchaguzi, jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TRW, Wallace Mayunga alisema NEC, Jeshi la Polisi wamefanya kazi nzuri ya kutoa elimu ya mpigakura hivyo wanamini uchaguzi utafanyika kwa amani, utulivu na haki.

Mayunga alisema, bado makundi mbalimbali yanapaswa kuendelea kufikiwa ili kupata elimu hiyo yakiwemo makundi ya wafugaji, wakusanya matunda na vijana.

“Tumeshuhudia kampeni za sasa zimekuwa za kistaarabu na kuwa kuna baadhi ya viashiria visivyo vizuri lakini vyombo vya dola vimeweza kukabiliana navyo kwa amani,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TRW, Justina Shauri aliwataka waandishi wa habari wawahamasishe wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu.

Shauri alisema kuwa taasisi yao itashiriki kutazama uchaguzi wa mwaka huu na wanaamini watakachokiona wataandika ripoti yake bila upendeleo na italisaidia taifa.

“Tumetoa elimu ya mpiga kura ili kuwawezesha watu wengi zaidi kushiriki kwenye uchaguzi utakawaweka madarakani viongozi wanaowataka.

Alisema rushwa ya uchaguzi ni tishio kwa chaguzi huru na haki, kwani rushwa ya aina hiyo inaleta viongozi wasio sahihi ambayo inapelekea kuwa na serikali ya kifisadi.

“Ni vyema tukaendelea kuhakikisha kampeni zikiwa huru na tulivu ambapo wagombea wa vyama vya siasa hawatatawaliwa na vitisho au rushwa.

Mayunga alisema, jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanywa na serikali kuhakikisha taasisi za umma na vyombo vya dola havitumiki katika namna ambayo vitachochea matokeo ya uchaguzi.

“Hata chama tawala kimetengwa kabisa na serikali na kwamba hakitumii vibaya nafasi yake kisiasa na kwamba vyama vyote vya siasa vinapewa fursa sawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles