26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Wadada wa kazi watakiwa kufuatilia elimu ya uzazi kukwepa mimba zisizotarajiwa

Na YOHANA PAUL, MWANZA

WASICHANA wanaofanya kazi za majumbani maarufu kama ‘dada wa kazi’ wameaswa kuzingatia elimu ya afya ya uzazi inayotolewa kupitia warsha, semina na vyombo vya habari ili kuepuka mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa.

Rai hiyo imetolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Wafanyakazi wa Majumbani (Wote sawa), Angela Benedicto, wakati akizungumza na gazeti la Mtanzania kuelezea juhudi zinazofanywa na shirika hilo kuwaelimisha wafanyakazi hao juu ya afya ya uzazi.

Angela alisema Shirika la WoteSawa mbali na kuwasadia mabinti wa kazi kuzijua haki zao pia wanawapatia elimu ya uzazi lengo likiwa ni kuwasadia wasichana hao kufahamu miili na afya zao na kujua jinsi gani wanaweza kujitunza kuepuka magonjwa ya zinaa, mimba za utotoni na mimba zisizotarajiwa.

“Tunaendelea kutoa elimu ya uzazi kwa wafanyakazi wa majumbani hivyo mimi napenda kuwaasa mabinti hawa wazingatie elimu hii tunayoitoa na inayotolewa na vyombo vya habari ili watambue wapo katika nyakati gani na inapotokea wamefanya ngomo isiyo salama wajue kuna madhara wanayoweza kuyapata.

“Kesi nyingi tulizonazo ni mabinti hawa kupewa mimba na vijana ambao ni watoto wa mabosi zao na hata wakati mwingine wanapewa mimba na kina baba wa familia na baadaye kutelekezwa lakini hayo yote ni matokeo ya  kukosa elimu ya uzazi.

“Niwaombe tu mabinti hawa wajaribu kufuatilia elimu ya uzazi ili wajikinge na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa lakini pia waajiri wao ambao wengi ni kina mama wajaribu kukaa na mabinti wa kazi na kuwaelimisha juu ya afya ya uzazi kwani ni kama watoto wao na wanapopata maambukizo ya magonjwa ya zinaa hata familia inakua haipo salama,” alisema Angela

Alisema iwapo mabinti hawa watapata uelewa mzuri wa afya ya uzazi hata wanapokuwa kwenye siku za hedhi watajua namna ya kujitunza kwa usafi hata pale wanapokuwa wanakaa na watoto pamoja na kutekeleza majukumu mengine.

Aidha mkurugenzi huyo wa WoteSawa alitoa wito kwa waajiri wa wasichana wa kazi katika siku ya  uchaguzi kuhakikisha wanawapa muda wafanyakazi wao kwenda kupiga kura ili watimize haki yao ya kikatiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles