26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Arsenali Yaibua Ushindi! Kweli Subira Huvuta Heri

Hivi juzi, timu ya soka ya Arsenali ambayo imechekwa kwa muda mrefu na wapinzani wake, imeweza kuibua ushindi katika mechi iliyoshuhudiwa na mamilioni ya watu duniani.

Mnamo Ijumaa, tarehe nne Machi mwaka huu, macho yote ya wapenda soka yalikuwa yameelekezwa katika uwanja wa Emirates huko London, ambako timu za Arsenali na Bournmouth zilikuwa zinamenyana. Mashabiki wengi pia waliitumia bet365 Tanzania bonus code ya michezo wanayoipenda mno.

Arsenali iliongoza Mfululizo?

Kusema kweli kulikuwa na huzuni kiasi kwa mashabiki wa Arsenali hapo mwanzoni, kwani kabla ya dakika moja kwisha kijana mmoja mchezaji wa timu ya Bournemouth aliweza kufunga bao la kwanza. Hapo ndipo mashabiki wa Arsenali walianza kushikwa na wasiwasi.

Hata hivyo, walitulia tu na kuendelea kuwashangilia wachezaji wa timu yao, wakijikumbusha vile wahenga walinena, eti “kutangulia sio kufika”. Roho zilikuwa zimetulia hapo Arsenali wakizidi kutawala uwanjani kwa kumiliki mpira, na kipindi cha kwanza kilichofikia kikomo, bao lilibaki lile lile moja tu.

Hapo basi, timu ya Arsenali ilikuwa na matumaini makubwa kwamba wangefunga bao hapo karibuni, na kuyasawazisha mambo. Mwenye kuifungia Bournemouth bao kipindi cha kwanza alikuwa ni mchezaji, Philip Billing, mzaliwa wa Denmark, mwenye umri wa miaka ishirini na sita.

Ingawaje bao la Billing liliwapa motisha wachezaji wenzake, timu ya Bournemouth haikuweza kujistahimili Arsenali, timu iliyo na uzoefu mkubwa wa kucheza katika mashindano makubwa. Kwa kifupi, Arsenali haikuongoza kwa mabao mfululizo, lakini mwishowe ndiyo timu iliyoibuka na ushindi.

Wenye Kufunga Mabao Uwanjani Emirates

Kipindi cha kwanza cha mapambano baina ya Arsenali na Bournemouth kiliisha kwa bao moja kwa sufuri, hapo timu ya Bournemouth ikitangulia. Mnamo dakika ya hamsini na saba, mchezaji wa Bournemouth, Marco Senesi aliifungia timu yake bao la pili, na hapo mashabiki wengi wakadhani kwamba hapo mwishowe Arsenali wangeona kivumbi.

Lakini, mambo yalibadilika kuanzia dakika ya sitini na mbili, ambapo mchezaji wa Arsenali, Thomas Partey, alifungia timu yake bao la kwanza. Ingawa mashabiki wa Bournemouth walitaka kuamini hilo lingekuwa bao la kutoa Arsenali machozi, hilo halikutimia. Mnamo dakika ya sabini, mchezaji Ben White aliifungia Arsenali bao la pili, na hapo kuweka timu zote mbili sambamba.

Muda wa Ziada: Arsenali Yafunga Bao La Ushindi!

Ilibidi timu za Arsenali na Bournemouth kucheza dakika za ziada, ili kubainisha mshindi. Mnamo dakika ya tisini na saba, nyota ya Arsenali iling’ara vilivyo, ambapo mchezaji, Reiss Nelson, aliifungia timu yake bao la ushindi.

Arsenali ilikuwa inashikilia uongozi katika michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza mwanzoni wa mchezo wa Emirates, and timu hii ilibaki bado inaongoza kwa meza ya michezo firimbi ilipolia. Timu hiyo ilipoondoka uwanjani siku hiyo, nyuso za wachezaji na mashabiki ziliwa zimeng’ara kweli kweli, timu iliyofuata kwa Ligi Kuu, Manchester City, ikiwa pointi tano nyuma ya Arsenali.

Yaliyotendeka Jumapili

Siku iliyofuata, Jumapili, tarehe tano Machi, timu ya Manchester United inayojulikana sana kama Man U ilipambana na timu ya Liverpool, na timu maarufu ya Man U ikalazwa bao saba kwa sufuri. Yamaanisha kwamba, mashabiki waliyoipendelea timu ya Liverpool walirudi manyumbani mwao wakiwa na tabasamu isiyo kifani.

Timu zingine zilizoshindana siku hiyo ni Nottingham Forest na Everton, na matokeo hapa yalikuwa bao mbili kwa mbili; yaani timu hizi mbili zilitoka sare. Mchezo uliopangwa kufuata siku ya Jumatatu, tarehe sita Machi, ni baina ya Brentford na Fulham.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles