27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Anthony atamba kupigana na Fury

anthony_joshuaLONDON, ENGLAND

BAADA ya bondia, Anthony Joshua, kushinda mwishoni mwa wiki katika pambano lake dhidi ya Charles Martin katika uzani wa Heavyweight, sasa ametamba kumpiga bingwa, Tyson Fury.

Joshua amekuwa na furaha kubwa baada ya kushinda taji hilo la IBF, lakini kwa sasa amesema kuwa lengo lake kubwa ni kupambana na Fury ili kuweka rekodi katika mchezo huo.

Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni bingwa wa Olimpiki, anaamini ana kila sababu ya kupigana na Fury.

“Ili niweze kutetea mataji yangu lazima nipigane na watu wenye uwezo, ninaamini kwa sasa naweza kupigana na Fury na nikashinda, ninaheshimu uwezo wake lakini katika ugumu chochote kinawezekana.

“Ubingwa wa IBF umezidi kunipa nafasi nzuri ya kupambana katika michezo mingine, hivyo naweza kusema nipo tayari kupambana na bondia huyo mwenye jina kubwa kwa sasa,” alisema Joshua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles