28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Andrey Coutinho kama Messi Yanga

Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam

KIUNGO mshambuliaji mpya wa timu ya Yanga,

Andrey Coutinho
Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho

, ni kama vile nyota wa Barcelona, Lionel Messi, kwa uwezo wa kutumia vyema mguu wa kushoto na kupiga mipira ya adhabu ndogo, huku akidai kuwa amekuja kusaka jina na mataji Tanzania.

Messi naye anatumia mguu wa kushoto na ni mtaalamu wa kupiga mipira ya adhabu ndogo na kona kama Coutinho, pamoja na kupiga mashuti ya kiufundi katika maeneo mazuri karibu ya lango la wapinzani.

Coutinho, 24, aliyeanza mazoezi jana na timu hiyo, tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili na kukabidhiwa jezi namba saba, iliyokuwa ikitumiwa na Didier Kavumbagu aliyetimkia kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC, ametua Yanga sambamba na Wabrazil wenzake, Marcio Maximo ambaye ni Kocha Mkuu na kocha msaidizi, Leonardo Neiva.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo jana asubuhi kwenye ufukwe wa bahari wa Coco, jijini Dar es Salaam, Coutinho, aliyekuwa akizungumza lugha ya Kireno tu na kocha Neiva kutafsiri kwa Kiingereza, alisema kupitia Yanga atafanikiwa kutengeneza jina na hatimaye kupata soko zaidi kwenye nchi kubwa duniani.

“Mimi nimekuja Tanzania kwa lengo pekee la kusaka jina na mataji, ili nipande chati na kucheza kwenye nchi kubwa duniani, Brazil kuna vipaji vingi sana, hivyo ni ngumu kutoka, ndiyo maana unaona Wabrazil wamesambaa kote duniani, kikubwa nawashukuru Watanzania wote na naamini nitaweza kutimiza hilo nikiwa hapa,” alisema Coutinho.

Akimuelezea Coutinho, aliyejiunga Yanga akitokea timu ya Castanhal EC iliyopo kwenye Ligi Daraja la Pili Brazil, Neiva alisema timu hiyo imepata mchezaji mzuri, kwani ana uwezo mzuri wa kumiliki mpira na kupiga mashuti, huku akieleza kuwa ni mtaalamu wa kupiga mipira ya adhabu ndogo.

“Coutinho anacheza winga ya kushoto na anatumia mguu wa upande huo, anaweza kufumua mashuti kama akiwa kwenye eneo zuri, vilevile ni mtaalamu wa kupiga mipira ya adhabu ndogo na pia ile ya kona,” alisema Neiva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles