Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Serikali imesema sheria inaruhusu hati ya kumiliki viwanja kuandikwa majina ya familia ikiwemo mume, mke pamoja na watoto hatua ambayo itasaidia kuondoa migogoro ya mirathi.
Akizungumza leo Jumamosi Desemba 19, mkoani Kilimanjaro. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliamu Lukuvi amesema kwa sasa wizara hiyo inasajili majina hayo na kwamba Watanzania watumie fursa hiyo vema kupunguza migogoro ya mirathi.
“Sisi katika wizara hii na serikalini humu tunapata shida sana ya kushughulikia mambo ya mirathi,wizara inakubali kusajili hati kwa majina zaidi ya mawili hata ukita baba,mama na watoto kusajili hati Moja inaruhusiwa hii inasaidia kuepusha matatizo ya miradhi hapo baadae,” amesema Lukuvi.
Aidha, Waziri Lukuvi ametoa wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu wa kufanya hivyo kutokana na kwamba keai nyingi za miradhi huwa na changamoto nyingi”alisema
“Kesi nyingi za mirathi wanakuja wajomba ambao hawakujua jasho lenu ambalo mmelichuma wanaandika hati wao wanajimilikisha hiyo ni fursa kwa wananwake…washawishini waume zenu wakati wa kuandika hati mje na majina yenu wote…hata kama umeoa wanawake watatu, sheria ipo wazi,ukija na jina la mtoto chini ya miaka 18 tutasajili jina lake na msimamizi wake.
“Ndoa zote tutaandikisha, akifa mke mmoja inafahamika kwamba haki iliyobaki ni ya wake wawili waliobaki na kwa upande wa mtoto akifikisha miaka 18 kunauwezekano wa kufuta majina ya awali ya wazazi na kumuachi mtoto,” amesema Lukuvi.
Aidha amesema utaratibu huo ikifiatwa hakutakuwa na vikao vya familia vya miradhi na migogoro isiyo ya lazima.
“Sio lazima kwamba mtu alitaka hati aje na mme wake zao Ila ni jukumu langu kuwalemisha kwamba Hilo linawezek,” amesema.