27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Andengenye akunwa utafiti taasisi za kilimo

Na Allan Vicent -Tabora 

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, amefurahishwa na maboresho makubwa yanayofanywa na taasisi za kilimo kwa wakulima wa mikoa ya Tabora na Kigoma.

Akizungumza wakati wa kilele cha maonyesho ya wakulima (Nanenane) Kanda ya Magharibi yaliyomalizika jana Uwanja wa Fatma Mwassa, Andengenye alisema utafiti na elimu iliyotolewa na taasisi hizo kumeleta tija kubwa kwa wakulima.

Alisema kuanzishwa vituo vya utafiti wa mazao, kumekuwa msaada mkubwa kwa  wakulima kutokana na ushauri mzuri wa kitaalamu, ubunifu na dhamira njema ya kuwainua wakulima.

Andengenye alitaja taasisi ambazo zimeleta mageuzi makubwa ya sekta ya kilimo na kuanza kunufaisha wakulima kuwa ni pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari), Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa (Tacri) na Kampuni ya Felisa.

“Tumejipanga vizuri ili kuhakikisha kilimo cha mazao ya kimkakati kinaendelea kupewa kipaumbele kikubwa wilaya zote za mikoa, ikiwemo kuboreshwa teknolojia na kusisitiza matumizi ya mbegu bora,” alisema Andengenye.

Alitoa wito kwa wadau na taasisi mbalimbali kuja kuwekeza katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika kanda hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Philemon Sengati alisema ndoto yake ni kuona maonyesho ya wakulima yanakuwa ya mfano wa kuigwa na kanda zingine na ikiwezekana mwakani maonyesho ya kitaifa yafanyikie hapo.

Alisema dhamira yake, ni kuona maonyesho ya ukanda huo yanakuwa mashamba darasa na bidhaa zote zinazoletwa ziwe na tija kubwa kwa wakulima, jamii, nchi na mataifa mengine.

Alitaja baadhi ya mazao ya kimkakati yanayolimwa katika ukanda huo, ambayo yamepewa kipaumbele kikubwa ni michikichi, kahawa, alizeti, korosho, pamba, tumbaku, mahindi, karanga, mpunga na mihogo.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles