25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

‘Ukomo wa hedhi huongeza magonjwa kwa wanawake’

Na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Honoratha Maucky amesema  ukomo wa hedhi kwa wanawake huongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MTANZANIA Dar es Salaam juzi, Dk. Maucky alisema hali hiyo hutokea kutokana na utengenezaji mdogo wa homoni za uzazi (oestrogen), hivyo kufanya mafuta mabaya kuwa mengi mwilini.

“Metabolick syndrome ni mkusanyiko wa vitu vinavyosababisha mtu kupata matatizo ya moyo, zinaweza kutokea kwa wanawake au wanaume, tofauti inatokea kwenye umri unavyokuwa mkubwa mwanamke  anakuwa  na  utengenezaji mdogo wa homoni za uzazi (oestrogen),  kinachotokea anakuwa na  mafuta  mabaya mengi.

“Hali hii humfanya kuwa na upungufu wa mafuta mazuri, uzito unaongezeka  kwa sababu hakuna uyeyushaji  wa mafuta  na yanabadilika,” alisema Dk. Maucky.

Alisema utafiti uliofanywa na American Heart Association, wanawake wengi hawafanyi mazoezi.

“Vihatarishi vya magonjwa ya moyo  (metabolic syndrome), tukiangalia American Heart Association  imeainisha  sababu za kuwa na dalili au hatari hizo.

“Sababu hizo ziko tano, tumetaja mafuta mazuri yakipungua, mafuta mabaya yakiwa mengi, ukiwa na sukari inayozidi pointi sita kabla hujala au kama una dawa ya kushusha sukari ni mojawapo ya sababu  inayotumika kujua kama kuna metabolic syndrome na vilevile uzito mkubwa, presha ya kupanda inayozidi 130-85.

“Ukichukua sababu hizi  na  kama ukipata sababu tatu kati ya hizo, unakuwa na methabolick syndrome, sasa hii iko kwa wanawake na wanaume, wengi ambao wamefikia kikomo cha uzazi  (menopause) au kuvuka wanaingia kwenye methabolic  syndrome zaidi,” alibainisha Dk. Maucky.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles