28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Amuli Mugisho kuachia nyimbo 3 za Kiswahili

KENTUCKY, MAREKANI

Mwimbaji mahiri wa Injili kutoka Marekani, Amuli Mugisho, ameachia video ya wimbo, Baba akianza kutekeleza ahadi ya kuachia nyimbo tatu za Kiswahili mfululizo.

Mugisho anayeishi mjini Lexington, Kentucky, amesema baada ya kutoa wimbo, Baba ataendelea kuachia nyimbo za Kiswahili lengo likiwa ni kuifikia jamii inayozungumza lugha hiyo na kuwafikishia ujumbe wa Mungu.

” Nimeachia video ya Baba ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube baada ya wiki moja nitatoa wimbo mwingine unaoitwa Raha Jipe Mwenyewe na baada ya wiki tena nitaweka mwingine unaitwa Kila Jambo na Wakati Wake, hivyo mashabiki wa Injili wajiandae kubarikiwa na nyimbo hizi za Kiswahili,” amesema Mugisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles