26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Teni, Davido kwenye kolabo ya kibabe!

Na Mwandishi Wetu

Msanii nyota nchini Nigeria, Teniola Apata a.k.a Teni amefanya kolabo ya heshima na staa wa Afrobeats, Davido katika kibao kipya For You.

Teni ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Vipaji nchini humo, Nigerian Talent Award, ameachia singo hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni safari ya kufyatua albamu mpya.

 Teni amesema: “For You ni wimbo ambao nimeufanya kusherehekea kiini cha upendo na uthibitisho kuwa kila wakati kuna mtu maalum ambaye anamaanisha ulimwengu kwako.

“Daima nilitaka kufanya rekodi kama hii na Davido hasa kwa sababu ya kumpongeza kama msanii, baba na mtu mwenye moyo mkubwa, mzuri uliojaa upendo. “

Kwa upande wa Davido, anasema: “Katika wimbo huu maalum, kama baba wa watoto wazuri watatu, naelewa ni kiasi gani wanamaanisha kwangu na ni kwa kiasi gani ninakuwa tayari kuwapa kila kitu kizuri ambacho dunia ipo tayari kuwapatia.”

Kibao hicho kitakuwa ndani ya albamu yake mpya , Wondaland ambayo itaachiliwa mwezi ujao imepikwa kwa miaka miwili katika majiji makubwa sita ya London, New York, Orlando, Ondo, Lagos na Abuja

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles