23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Amkata mpwa wake sehemu za siri

NA AMON MTEGA, SONGEA

MKAZI wa Kijiji cha Majimaji kilichopo Tunduru mkoani Ruvuma, Patrick Vitus (70), amekatwa sehemu zake za siri na kuachwa zikining’inia.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kwa njia ya simu jana, Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Hussein Mkali, alisema Patrick alikatwa sehemu zake hizo na mpwa wake Zainabu Said (32), baada ya kumkatalia kwenda kumfuata mumewe aliyekuwa kwa mke mdogo.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tisa usiku katika maeneo ya mashamba ya kijiji hicho ambako walikuwa wakifanya shughuli za kilimo.
Alisema mume wa Zainabu ni Musa Said (40), aliyeenda kulala kwa mke mwingine ambaye jina lake halikupatikana na kumsababishia Patrick kukatwa sehemu zake za siri.

Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo, ofisi ya kijiji imemkamata Zainabu na kumpeleka polisi ambako ndiko maelezo zaidi ya kuhusiana na tukio hilo
yatatolewa huku Patrick akiwa amepelekwa Hospitali ya Tunduru.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, alisema atatoa ufafanuzi wa tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles