28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Amitabh Bachchan ashinda tuzo ya Bollywood

amitabh-bachchan_625x300_51410169839NEW DELHI, INDIA

NYOTA wa filamu nchini India, Amitabh Bachchan, amefanikiwa kushinda tuzo ya mwigizaji bora nchini India katika tuzo za kitaifa za Bollywood kutokana na filamu yake ya ‘Piku’.

Katika tuzo hizo zinazotolewa kila mwaka na Serikali ya India, upande wa wanawake, nyota wa filamu ya Tanu Weds Manu Returns, Ranaut, alifanikiwa kutwaa tuzo hiyo.

Tuzo nyingine ikiwemo filamu bora imechukuliwa na Bahubali, huku Sanjay Leela Bhansali akijishindia muongozaji bora wa filamu ya ‘Bajirao Mastani’.

“Nimekuwa na furaha kubwa kutwaa tuzo hiyo, ninaamini watu wameona nini nilikifanya katika filamu hiyo na ndio maana nikawa mshindi, kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika filamu hasa kutokana na wasanii wapya ambao wanafanya vizuri,” alisema Bachchan.

Hiyo inakuwa tuzo ya nne kwa Bachchan. Awali aliwahi kutwaa tuzo ya uigizaji bora wa mwaka 1990, 2005 na 2009.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles