26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Amitabh Bachchan akanusha kutolipa kodi

Amitabh-BachchanNEW DELHI, INDIA

NYOTA wa filamu za Bollywood nchini India, Amitabh Bachchan, amekana kuhusishwa na kampuni zozote za kigeni anazotumia kukwepa kulipa ushuru.

Mtandao wa India Express umetoa taarifa kwamba, Bachchan aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa kampuni nne za kigeni mwaka 1993, zilizosajiliwa nchini Uingereza kwenye visiwa vya Virgin na Bahamas.

Yeye na nyota mwenzake wa kike, Aishwarya Rai, ni miongoni mwa Wahindi 500 walioorodheshwa katika gazeti la Panama kwamba wanakwepa kulipa kodi.

Hata hivyo, nyota huyo wa filamu amekana kujihusisha na ukwepaji kodi kama inavyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini humo.

“Kikubwa ni kwamba uchunguzi ufanyike ili kujua ukweli wa jambo hilo, lakini ninaamini kwa upande wangu hakuna ukweli juu ya jambo hilo,” alisema Bachchan.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles