24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

Shika ndinga ya EFM kuanza kesho

EFMMNA ASIFIWE GEORGE

SHINDANO la shika ndika linaloendeshwa na Redio EFM litaanza kuchezeshwa kesho.

Ofisa Habari wa EFM, Aneth Mrindoko, alisema shindano hilo litawahusisha wakazi wa Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni pamoja na wakazi wa Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya Bagamoyo na Kibaha.

“Mwaka huu EFM inalisongesha kwa kutoa zawadi ya magari mawili aina ya Suzuki carry pamoja na pikipiki aina ya boxer ili kuendelea kuwa karibu na wasikilizaji wake kama ilivyotoa zawadi ya gari mwaka jana.

“Washiriki 40 kutoka kila wilaya watatakiwa kushiriki nusu fainali na baadaye washiriki 10 watakaopita watapata nafasi ya kushiriki katika fainali za mwisho kutoka kila wilaya na hatimaye washindi wawili wa kwanza mwanamke na mwanamume wataibuka na ndinga na wengine kuibuka na pikipiki.

“EFM Redio hufanya shindano hili kwa lengo la kuwawezesha wasikilizaji wake kuongeza na kukuza kipato kitakachochangia kuimarisha maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,577FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles