28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Amcos, Wanunuzi wa pamba waiomba serikali kuangalia upya kodi ya zuio

Na Derick Milton, Simiyu

Vyama vya Msingi vya Ushirika pamoja na wanunuzi wa zao pamba mkoa wa Simiyu, wameiomba Serikali kuangalia upya kodi ya zuio asilimia 2 ambayo ni mpya iliyowekwa katika mazao ya kilimo ikiwemo pamba, uvuvi na mifugo.

Wamesema kuwa ni vyema kodi hiyo ingeliwekwa katika zoezi la kupanga bei ya pamba, ambalo ufanyika kabla ya msimu mpya wa ununuzi wa zao hilo kufanyika ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wakulima.

Vyama hivyo vya msingi pamoja na wanunuzi wametoa ombi hilo wakati wa semina iliyofanyika jana mjini Bariadi na maofisa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kuwaelimisha juu ya kodi hiyo.

Awali, akizungumza katika semina hiyo Kaimu Meneja TRA Mkoa, Marko Nsobi, alisema kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo, ya kodi ya zuio anayetakiwa kuilipa ni mnunuzi wa pamba baada ya kuzuia asilimia 2 ya malipo ambayo anatakiwa kumlipa Amcos.

Alisema kuwa manunuzi wa pamba anapokwenda kwenye Amcos kwa ajili ya kununua pamba, anatakiwa kuzuia asilimia mbili ya malipo ya pamba ambayo ameichukua kwenye Amcos hiyo.

“Kinsingi kodi hii mkulima hatakiwi kuilipa wala Amcos na yeye hatakiwi kuilipa, ila wao watapokea ela pungufu baada ya mnunuzi kukata kodi hiyo kwenye malipo ambayo anatakiwa kuilipa Amcos baada ya kuchukua pamba,” alisema Nsobi.

Daniel Singiri mmoja wa viongozi wa Amcos alisema kuwa uwepo wa kodi hiyo ni muhimu kwani inakwenda kuleta maendeleo ya nchi, ambapo ameomba kufanyiwa marekebisho katika utekelezaji wake.

Alisema kuwa kodi hiyo kuletwa katikati ya msimu huku serikali ikiwa tayari imetoa bei elekezi ya kununua pamba, itawatesa wakulima kwani watapokea kiasi pungufu ya pamba ambayo watakuwa wamepeleka Amcos.

Aidha Singiri ameongeza wakulima wanatakiwa kupewa elimu zaidi juu ya kodi hiyo mpya, ili kuweza kufahamu msingi wake na kuondoa malalamiko ambayo wanaweza kutoa pindi watakapokea malipo pungufu.

“Lengo la serikali kuleta kodi hii siyo mbaya, maana ni katika kuleta maendeleo ya nchi yetu, lakini muda ambao kodi imeletwa ndiyo tatizo, katikati ya msimu inaleta shida, tunaiomba serikali ni vyema kodi hii ikaanza utekelezaji wake msimu mpya wa pamba,” alisema Singiri.

Naye James Mbulu kutoka Alliance Ginnery ugumu upo katika utekelezaji wa kodi hiyo kwani wanunuzi wengi wamekuwa wakipeleka pesa kama kianzio kwa Amcos na wakulima wamekuwa wakipwa pesa zao kamili.

“Ikiwa tutapeleka kianzio na wakulipwa pesa zote kamili bila ya kuwakata asilimia mbili itakuwa ngumu Amcos kumudu hilo deni, ni vyema elimu ikatolewa zaidi hasa kwa wakulima, lakini pia hii kodi iwekwe katika mkokotoo wa bei ya pamba,” alisema Mbulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles