27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Machifu wampa jina jipya Rais Samia

Jescar Victor,TUDARCO

Umoja wa Machifu Tanzania, umempa jina la Hangaya lenye maana ya nyota ya asubuhi inayong’aa, Rais Samia Suluhu Hassan leo Septemba 8, wakati alipozindua tamasha la utamaduni la machifu jijini Mwanza.

Akizungumza katika tamasha hilo, Rais Samia amesema ni mara yake ya tatu kushiriki katika tamasha la utamaduni na anaushukuru umoja wa Machifu kwa kumpatia jina hilo jipya la Hangaya.

Aidha, amemnukuu Hayati Dk. John Magufuli kwa kusema kuwa: “Utamaduni ni kiini au roho ya Taifa lolote, Taifa lisilo na utamaduni ni sawa na watu wasio la roho kwa sababu utamaduni ni mojawapo kati ya mambo muhimu yenye kutambulisha Taifa.

Pia lugha ya kiswahili ni lugha inayotutambulisha taifa, zaidi ya hapo utamaduni unatusaidia kueleza historia, mila na desturi za jamii ya taifa husika.

Rais Samia amewapongeza viongozi wa umoja wa watemi wa kisukuma kwa kuweza kuandaa tamasha hilo la kwa niaba ya umoja wa machifu wa Tanzania na kusema  amejenga imani kuwa Watanzania wamejifunza mengi kama vile tamaduni, mila na desturi mbalimbali za kabila la wasukuma pamoja na kuhamasisha makabila mengine ya Tanzania kutangaza tamaduni zao na kufanya mashindano katika makabila hayo.

Ameeleza kuwa utamaduni ni biashara na ni chanzo kikubwa cha kipato kwani ni kivutio kikubwa cha utalii kama ilivyo kwa nchi za Japani, Asia, Ethiopia na Indonessia.

Pia ameeleza kuwa, moja kati ya vitu vinavyoifanya nchi ipokee idadi ndogo ya watalii na wengine wanaokuja wasiweze kurudi tena nchini ni kutokana na wigo mdogo wa shughuli za kitalii kwani utalii  umejikita zaidi kwenye maliasili, wanyama na misitu hivyo inafanya watalii wanaokuja nchini kukaa kwa siku chache.

“Serikali inapanua wigo wa utalii ikiwamo utalii wa utamaduni kwani wiki nzima nimekua nikizunguka kuandaa program ya filamu ya fursa na vivutio mbalimbali vya kiuchumi hapa nchini na mojawapo ya vivutio vinavyotangazwa ni utamaduni wetu.

 “Pia inakusudiwa kutangazwa kwa fursa zote za kiutamduni tulizonazo. Vilevile katika risala ya kiongozi wa umoja wa watemi wa wasukuma na kwa niaba ya umoja wa machifu Tanzania umewasirisha baadhi ya changamoto zinazoikabili katika kutekeleza shughuli za kila siku ikiwemo ombi la kutambulishwa rasmi kwa umoja wa machifu Tanzania,”amesema Rais.

Raisi Samia amesema serikali imeanzisha mfuko wa sanaa na utamaduni wenye bajeti ya shilingi bilioni 1.5 ambapo mpaka sasa upo kwenye mchakato wa kuandaa sera mpya ya utamaduni.

Aidha  amesema  suala la Corona machifu ndiyo watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii hivyo ishirikiane na serikali kuwahimiza watanzania kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles