26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Amber Rose adondosha chozi kisa Kanye West

amber-rose-kanye-westLOS ANGELES, MAREKANI

ALIYEKUWA mpenzi wa zamani wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, Amber Rose, juzi alidondosha
chozi baada ya kukumbuka maneno ya Kanye West pindi walipokuwa wapenzi.

Februari mwaka huu Kanye West kupitia radio ya Power 105.1 kwenye kipindi cha The Breakfast Club ya nchini Marekani, alisikika akisema kuwa ‘Ni vigumu kuishi na mwanamke kama Amber Rose, hata wanawake wenzake inakuwa ngumu, baada ya kuachana naye nilitumia nusu saa kumfikiria Kim Kardashian.’

Mrembo huyo alikumbuka kauli hiyo alipokutana na wanawake mbalimbali jijini Los Angeles kwa ajili ya kujadili
maendeleo ya wanawake badala yake akajikuta akibubujikwa na machozi

“Siwezi kumsahau Kanye West kutokana na maneno yake, lakini nimemsamehe kwa kuwa mimi nibinadamu, nilimpenda lakini hatukudumu,” alisema Amber Rose.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles