31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEUA MKE,WATOTO AHUKUMIWA KUNYONGWA

Na   Walter   Mguluchuma-Katavi .

MAHAKAMA Kuu Kanda ya  Sumbawanga, imemhukumu   Yustine   Robarti (32)mkazi  wa   Kijiji  cha    Majimoto   Wilaya  ya  Mlele   Mkoa  wa   Katavi  kunyongwa  hadi  kufa,   baada  ya  kutiwa hatiani kwa kosa la   kumuua    mke  wake  na   watoto wake wawili, kisha  kuwatumbukiza  ndani ya kisima  cha  maji .

Hukumu   hiyo  ilitolewa  wiki iliyopita  na   Jaji wa mahakama hiyo,  Adam Mambi katika vikao vinavyoendelea kufanyika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Mtuhumiwa alitiwa hatiani,  baada ya  mahakama  kuridhika  na      ushahidi  uliotolewa  na  upande  wa  mashtaka  uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Achiles Mulisi.

Awali katika kesi hiyo,Mulisi alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 23,2015 saa 7 usiku baada ya kutokea  ugomvi na mke wake, wakati wakiwa wamelala chumbani na watoto wao wadogo ambao aliuawa.

Ilidaiwa siku ya tukio, Yustini alimpiga mke wake, Monica Lwiche (25), kisha baada ya kumuua alimtupa  ndani ya  kisima cha maji.

Baadae aliwauwa  watoto wake, Eliza Robert (4) na Frank Robart (6) kwa lengo la kuvuruga ushahidi kwakuwa wakati akifanya kitendo hicho  watoto walikuwa wakishuhudia

Kabla ya kufanya tukio hilo, mshtakiwa alikuwa ametoa kauli za vitisho endapo mke wake atarudi nyumbani atafanya jambo litakalokuwa la kihistoria na ambalo halitasahaulika  kwa wakazi wa kata hiyo.

Mshtakiwa katika kesi hiyo, alikuwa anatetewa na wakili Patrick Mwakyusa ambapo upande huo wa utetezi ulikuwa na mashahidi wawili, mshtakiwa mwenyewe na baba yake mzazi.

Katika utetezi huo, waliiomba mahakama imwachie huru kwani upande wa mashtaka umeshindwa kudhibitisha kama kweli alitenda kosa hilo.

Pia walidai  upande wa mashtaka, umeshindwa kudhibitisha kuwa wakati anafanya mauaji hayo, hakuna mtu yoyote aliyeshuhudia tendo hilo la kumuua mke wake na watoto.

Utetezi huo ulipingwa vikali na Mulisi kwa kile alichodai  wa katika ugomvi unatokea  mwanzoni, mama mwenye nyumba alikokuwa amepanga mshtakiwa  alishuhudia ugomvi huo na ushahidi wa  maneno ya vitisho aliyoyatoa mshtakiwa ni ushahidi tosha ndiye aliyetekeleza mauaji hayo.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Adam Mambi  aliiambia mahakama  kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka na utetezi mahakama, lazima iangalie mambo  matatu ambayo ni ushahidi wa mazingira,je upande wa mashtaka unadhibitisha na kama kweli  mshtakiwa amehusika au la.

Hivyo aliieleza mahamakama kuwa kutokana na maswali hayo,mahakama ilihoji na kujilisha na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Kutokana na ushahidi huo, mahakama ilimtia Robert kwa kosa la kifungu cha sheria namna 196 na 197 cha kanuni ya adhabu na alitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kabla ya kusoma hukumu.

Naye Mwasheria wa Serikali, aliiomba mahakama itoe adhabu kali li iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo na hasa wanaowaua watu wasiokuwa na hatia.

Baada ya maelezo hayo,Mambi ali alimhukumu kunyongwa hadi kufa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles