29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEMUHUKUMU SUGU AENDA LIKIZO

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA

HAKIMU Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite, ameanza likizo.

Hakimu Mteite alianza likizo juzi baada ya kumhukumu  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), maarufu kwa jina la Sugu,   kwenda jela miezi mitano baada ya kupatikana na hatia ya kumkashfu Rais Dk. John Magufuli.

Katika hukumu hiyo, Sugu alikwenda jela na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga ambaye naye alipatikana na hatia katika shtaka hilo.

Akizungumzia likizo hiyo, Hakimu Mteite alisema ni haki yake kupumzika na kwamba hiyo ni likizo ya kawaida ya mwaka.

“Kwanza kabisa  nimeshangazwa na taarifa za upotoshaji zinazoendelea kusambazwa kwenye mitandao ya  jamii kwamba nimechukua likizo eti kwa sababu nimemhukumu Sugu kwenda jela.

“Kwanza kabisa  ieleweke kwamba, likizo ni haki ya mtumishi na ipo kwamujibu wa sheria, pia ni utaratibu wa ofisi kwa mtumishi yeyote kupata muda wa mapumziko.

“Sifanyi kazi kwa kuongozwa na maneno ya watu, nafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria na Katiba ya nchi inavyosema.

“Hao watu waache waseme wanavyotaka, lakini ukweli ni kwamba  likizo niliyochukua ni ya kawaida kabisa na mwajiri wangu alikuwa anaifahamu kwa sababu muda wangu wa kuanza likizo ulikuwa umeshafika.

“Hata ukiangalia rekodi zangu za likizo zimeweka bayana ni kipindi gani huwa napumzika, hivyo nawashangaa watu wanavyohoji,”alisema Hakimu Mteite.

Naye Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, George Herbert, alikiri mtumishi huyo kuanza likizo  ingawa hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani.

“Ni kweli hakimu huyo ameanza likizo yake ya mwaka kama ilivyo kwa watumishi wengine wa Serikali.

“Lakini, uelewe kwamba sipendi kuzungumzia masuala binafsi ya mtu kwa sababu hata likizo ni suala binafsi la mtu,” alisema Msajili Herbert.

Wakati huo huo, mawakili wa Mbunge Sugu waliokuwa wakihaha kukata rufaa dhidi ya wateja wao hao, wanaendelea kukamilisha taratibu za kukata   rufaa.

Mmoja wa mawakili hao, Faraji Mangula, aliiambia MTANZANIA jana kwamba walikuwa wameshapata nakala ya hukumu kwa ajili ya maandalizi ya kukata rufaa.

“Nakala ya hukumu tunayo na rufaa tumeshakata, lakini, kuna mambo madogo madogo tunayakamilisha kabla hatutapeleka nyaraka zetu mahali husika,” alisema.

ALICHOSEMA MBOWE

Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema hukumu dhidi ya Sugu inalenga kufifisha demokrasia katika Mkoa wa Mbeya.

“Tunaiheshimu mahakama kwa sababu  ndiyo mhimili unaoweza kuisaidia nchi katika kutenda haki, lakini tunakwazwa na vitendo vya baadhi ya mahakimu.

“Hatuwezi kusema hatuna imani na mahakama na wala hatutaiingilia kama itafanya kazi yake kwa weledi, lakini tutaizungumzia   inapoonekana haitendi haki.

Inaendelea…………… kwa maelezo zaidi pata nakala yako ya Gazeti la #MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles