25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ajinyonga kuogopa kuleta aibu ndani ya familia

Na Malima Lubasha, Serengeti

MSICHANA Rebeca Chacha (16) Mkazi wa kijiji cha Matare Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa madai ya kupata ujauzito hali ambayo ingeleta aibu katika familia kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la Wakurya.

Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Serengeti, ACP Kabengwe Mathias amethibitisha kutokea tukio hilo amba lo limetokea Julai 7, mwaka huu saa 3:00 asubuhi katika kitongoji cha Manyunyi sehemu ya mtoni alipokwenda kuchota maji.

Kamanda Mathias amesema uamuzi wa binti huyo kujiondoa uhai kwa kujinyonga ameuchukua yeye mwenyewe bila kugombezwa na mtu yeyote jambo ambalo siyo sahihi, hivyo Jeshi la Polisi limeona hakuna dalili ya kishuku mtu wa kuhusika na kuwaonya wananchi kutojichukulia sheria mkononi hali iliyosababisha msichana huyo kupoteza maisha kwa kujinyonga.

Awali, Chacha Mnata ambaye ni baba mzazi wa marehemu alisema binti yake aliugua na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ambapo katika uchunguzi wa daktari alibainika kuwa na malaria na damu imepungua mwilini hivyo alitibiwa na kurudi nyumbani.

Mzee Chache ameendelea kuongeza kuwa: “Akiwa hapa nyumbani mama mzazi wa binti aliona mabadiliko ya mwili, matiti yamekuwa makubwa yamevimba tofauti na alivyokuw,a hata hivyo binti alikana kuwa na mimba.

“Mama yake aliendelea kumbana aseme ukweli hatimaye alikubali ana ujauzito lakini hakumtaja kijana aliyempa na aliendelea kufanya kazi za nyumbani za kuosha vyombo na kuchota maji mtoni kama kawaida na siku ya tatu alifuata maji mara mbili na mara ya tatu alikwenda mtoni na kukaa huko zaidi ya saa tatu bila kurudi hali iliyompa wasiwasi mama na kuamua kufuatilia na kukuta ndoo pekee,” amesema Chacha ambaye ni baba wa marehemu.

Mwili ulivyogundulika

Naye shuhuda wa tukio hilo, Chacha Mohono ambaye ni mmiliki wa shamba la miwa amesema vijana wawili walikwenda hapo shambani kwake kununua miwa na baada ya ununuzi kufanyika walichepuka kwenda kutafuta kamba za kufungia miwa ndipo walikuta mwili wa binti huyo unaning’inia juu ya mti akiwa amejinyonga tayari.

Amesema walipouangalia kwa makini walikuta binti huyo akiwa tayri amefariki dunia ndipo wakapiga yowe na watu kujitokeza na ndipo jeshi la polisi likaarifiwa.

Katika hatua nyingine Kamanda Mathias amewaonya wananchi  kuacha tabia ya kujihusisha na upikaji wa pombe haramu ya gongo ambayo inasababisha mauaji mengi wakisha kunywa pombe hiyo  na kwamba atafanya msako kwa wale wote watakaobainika wanapika.

Kamanda Mathias alisisitiza kuwa kinywaji hicho haramu kinachangia kuharibu akili za watu wengi kwani imefikia wakati kuboreshwa kwa kuchanganya vitu vingine kama vile bangi na kemikali nyingine baada ya kutumia na kuanzisha ugomvi bila sababu hata kutokea mauaji.

Amewasihi wananchi kupiga vita gongo kwani pia imechangia wazazi kutozungumza na watoto wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles